TERRAZZO
Terrazzo ni material inayotumika kwenye ujenzi ambayo hutengenezwa kwa vipande vidogo vidogo sana(suitable chips), ambavyo hutokana na madini ya marble, quartz, granite au glass. Vipande hivyo huchanganywa na binder ambayo ina cement au kemikali au mchanganyiko wa vyote viwili. Terrazzo inapowekwa kwenye sakafu huwa inapigwa polish ili ing’ae na kuwa murua. Terrazzo huwa inachanganywa na pigments ambazo huwa na rangi tofauti-tofauti.
sakafu ya terrazzo
Mara nyingi terrazzo huwekwa
kwenye sakafu ya zege, yenye kina cha walau milimita 75. Kabla ya kuweka
terrazzo huwekwa kwanza zege laini ya milimita 25. Kabla zege laini
halijakakamaa, huwekwa vipande vya chuma au plastic(divider strips) ili iwe
igawanye sakafu kwenye vipande-vipande, ndio maana sakafu ya terrazzo huwa
inaonekana ipo kwenye patterns za rangi tofauti-tofauti.
sakafu ya terrazzo yenye rangi tofauti-tofauti
Pattern hizo huwa zinasaidia sana wakati wa
kutanuka na kusinyaa kwa sakafu ili isitoe ufa. Terrazzo inaweza kutumika katika
jengo la aina yryote ile. Inaweza kutumika kwenye nyumba za ibada, nyumba za
makazi, biashara, ,ikusanyiko n.k.
sakafu ya terrazzo
0 comments:
Post a Comment